Kitaaluma, Askofu Dag Heward-Mills ni mwuguzi na mwanzilishi wa Umoja wa Madhehebu yatokayo Kundi la Makanisa ya Lighthouse. Umoja wa Madhehebu yatokayo Kundi la Makanisa ya Lighthouse unahusisha makanisa elfu tatu yanayoongozwa na wachungaji wenye uzoefu walioandaliwa na kufundishwa kutoka ndani. Askofu Dag Heward -Mills anasimamia kundi hili la dhehebu la kikarismatiki, ambayo yanaendelea katika katika zaidi nchi 90 katika bara la Afrika, Asia, Ulaya, Carribea, Australia, Marekani Kaskazini na Kusini.
Akiwa katika huduma zaidi ya miaka ishirini na tano, Dag Heward-Mills aliandika vitabu vingi vinavyouzika sana ikiwamo ‘Stadi ya Uongozi’, ‘Uaminifu na Ukosefu wa Uaminifu’, na ‘Kanisa Kubwa’. Anajulikana kuwa mwandishi mwenye vitabu vingi katika Afrika, akiwa na vitabu vyake vilivyotafsiriwa katika zaidi ya lugha 50 pamoja na nakala zaidi ya milioni 20 zilizochapishwa
-
Kila mtu anayethubutu kuanzisha na kutengeneza kazi yoyote mpya huongozwa na tamanio la dhati kuona kazi hiyo ikiendelea na kudumu. Kwa nini kazi yako isidumu? Biblia inatuhimiza tuchukue jukumu la kuzaa matunda yadumuyo. Katika Nguzo za Uaminifu, utapata maarifa ya kina ya kibiblia, hekima ya vitendo, na kanuni imara zinazouimarisha uongozi, mahusiano ya kudumu, pamoja na mafanikio ya kudumu katika huduma. Hiki ni kitabu cha lazima kwa yeyote anayetamani kujenga huduma au maisha yatakayodumu hata mbele ya majaribu ya muda. -
Kitabu hiki kinakuacha ukiwa huna shaka kwamba Mungu anatuita kwenye uaminifu. Uaminifu ni takwa la Mungu kwetu! Kitabu hiki chenye mvuto kinajibu waziwazi swali “Kwa Nini Uaminifu?” Ikiwa umewahi kujiuliza kuhusu hitaji la uaminifu, maarifa haya yenye nguvu ya kibiblia yanaangazia jinsi uaminifu unavyoimarisha makanisa, hujenga huduma za kudumu na kukuza umoja miongoni mwa waumini. Baada ya kusoma kitabu hiki cha muhimu, cha mwandishi maarufu anayeuzwa zaidi, Dag Heward-Mills hutakuwa na shaka kuhusu somo muhimu zaidi la uaminifu. -
Uasi si kosa tu - ni kosa kubwa machoni pa Mungu! Uasi ni roho inayokaidi mamlaka na kwenda kinyume na utaratibu uliowekwa na Mungu. Ni mzizi wa machafuko na unaweza kukuongoza kwenye kiza kinene cha maisha na huduma, ikiwa utairuhusu katika maisha yako! Kumbuka, uasi ulikuwa dhambi ya kwanza kuwahi kuandikwa katika Biblia! Uasi ulimchukua malaika wa nuru na kumbadilisha kuwa shetani. Hiyo ndiyo nguvu ya uasi! Ni hatari, ni yenye hila na itakuharibu ikiwa utairuhusu kuota mizizi ndani yako. Katika kitabu hiki, utagundua jinsi ya kutambua aina mbili za uasi zilizofichika na zilizo wazi ambazo zinaweza kuingilia maisha yako au huduma yako. Usichukulie kijuu juu! Viondoe miongoni mwenu! -
Biblia inauliza swali hili la muhimu sana: "Ni nani awezaye kumpata mtu mwaminifu?" Hili linaonyesha jinsi ilivyo vigumu kumpata mtu mwenye sifa ya thamani sana iitwayo “uaminifu.” Je, umewahi kujiuliza kwa nini watu wengine huanza safari yao ya Kikristo kwa ari na shauku, lakini huanguka njiani? Kwa nini wengine huanza kwa moto wa huduma lakini huishia katika uharibifu? -
Heshima ni jambo muhimu ambalo kila mtu anahitaji kujua. Kuheshimu ni amri ya kibiblia. Heshima ni muhimu sana katika uhusiano wako na Mungu. Heshima ni muhimu sana katika uhusiano wako na nabii wako, mchungaji wako, mume wako na watu wengine wenye mamlaka. Usipompa heshima anayestahiki heshima, kamwe hutakuwa na uhusiano sahihi na watu fulani. -
Msengenyaji ni mtu anayetoa taarifa za uongo na za kuharibu kuhusu mtu mwingine, kwa kawaida kwa lengo la kuharibu sifa ya mtu huyo. Usengenyaji mara nyingi huendeshwa na chuki na nia mbaya. Msengenyaji wa kazi ya Mungu na wa watumishi wa Mungu huwa na agenda ya kishetani ya kupunguza ushawishi na huduma ya mtumishi wa Mungu na pia kuharibu sifa ya Kanisa na watumishi wa Mungu. Katika enzi hii ya mitandao ya kijamii, usengenyaji umetumika kama silaha ya kuwaangamiza watu na kuchafua sifa zao walizojitahidi kuzijenga. Katika kitabu hiki cha kufumbua macho, utajifunza mbinu za wasengenyaji na utapata faraja katika uhakika wa hukumu ya Mungu dhidi yao. Kwa mafundisho haya kutoka kwa Dag Heward-Mills, utainuka juu ya upinzani na kuwa mhudumu wa injili asiyezuilika! -
Yesu Kristo ndiye Nabii mkuu zaidi aliyepata kuishi! Alitabiri kwamba maumivu na makwazo yatakuja kwa kila mmoja. Maumivu na makwazo yamesababisha uharibifu mkubwa sana katika kanisa. Ni ombi langu kwamba kwa maneno haya machache utaokolewa kutoka kwa uovu na laana inayokuja kwa njia ya kwazo. Tena, zaidi ya hayo, mwanangu, uwe na maonyo: kutunga vitabu vingi hakuna mwisho; na kusoma sana ni uchovu wa mwili! -
Unapofikiria jina "Yuda" unafikiria usaliti na mtu aliyemfanyia Yesu uovu. Marejeo ya Yuda katika Biblia, hayakosi kuongeza kwamba alimsaliti Yesu. Je, haishangazi kutambua kwamba Yuda alikuwa rafiki wa Yesu? Yuda alikuwa mmoja wa wale waliochaguliwa. Yuda alikuwa mshiriki wa karibu wa timu hiyo. Ili kukidhi vigezo vya kuwa Yuda Iskarioti, ni lazima uwe karibu na Yesu, karibu na uongozi au uwe juu sana katika uongozi. Kifungua macho kweli! Ufichuzi huu wa hivi karibuni wa mwandishi mashuhuri, mchungaji na msemaji wa mikutano Dag Heward-Mills, utafichua kila Yuda aliye miongoni mwenu. -
Wachungaji wengi waliofadhaishwa wamejiuliza swali hili: “Kwa nini kanisa hili Halina maendeleo?” Unautambuzi wa hili swali, sivyo? Unaweza kuwa mchungaji mpya aliyeteuliwa, mmisionari kwa mataifa, mchungaji anayeanzisha tawi la kanisa lenye mafanikio… orodha inaendelea! Hili ni swali ambalo wengi wetu tunahitaji jibu.Katika mtindo wake wa kawaida, wa vitendo na uhalisia, mwandishi anayeuzwa sana Dag Heward-Mills, anashughulikia swali ambalo limekuwa likiomba jibu. Hili ni jambo la lazima kusomwa kwa mtu yeyote anayechunga kanisa; yeyote ambaye ana nia ya kushiriki injili ya Yesu Kristo na kuwakusanya watu kwa Mungu. -
Dag Heward-Mills ni mwandishi wa vitabu vingi, ikiwemo kitabu kinachouzwa sana "Uaminifu na Ukosefu wa Uaminifu". Yeye ni mwanzilishi wa dhehebu lenye makanisa zaidi ya elfu moja linaloitwa "The Lighthouse Chapel International". (Kanisa la Kimataifa la Lighthouse). Dag Heward-Mills, mwinjilisti wa kimataifa huhudumu katika Mkutano wa Injili wa Kimataifa na Yesu Mponyaji na mikutano duniani kote. kwa taarifa zaidi, tembelea www.daghewardmills.org. -
Usiku mmoja, wakati akiwa ni mwanafunzi wa utabibu katika mji mmoja huko Ghana, katika hali ya mwujiza Mungu alimpaka mafuta Dag Heward-Mills wakati alipokuwa akimsubiri Bwana. Alipakwa mafuta kwa namna isiyo ya kawaida na kusikia maneno, “Tangu sasa na kuendelea unaweza kufundisha…” Wito huu usio wa kawaida ndio uliomwongoza kwenye huduma iliyosambaa duniani kote.