Mwandishi

 

Kitaaluma, Askofu Dag Heward-Mills ni mwuguzi na mwanzilishi wa Umoja wa Madhehebu yatokayo Kundi la Makanisa ya Lighthouse. Umoja wa Madhehebu yatokayo Kundi la Makanisa ya Lighthouse unahusisha makanisa elfu tatu yanayoongozwa na wachungaji wenye uzoefu walioandaliwa na kufundishwa kutoka ndani. Askofu Dag Heward -Mills anasimamia kundi hili la dhehebu la kikarismatiki, ambayo yanaendelea katika katika zaidi nchi 90 katika bara la Afrika, Asia, Ulaya, Carribea, Australia, Marekani Kaskazini na Kusini.

Akiwa katika huduma zaidi ya miaka ishirini na tano, Dag Heward-Mills aliandika vitabu vingi vinavyouzika sana ikiwamo ‘Stadi ya Uongozi’, ‘Uaminifu na Ukosefu wa Uaminifu’, na ‘Kanisa Kubwa’. Anajulikana kuwa mwandishi mwenye vitabu vingi katika Afrika, akiwa na vitabu vyake vilivyotafsiriwa katika zaidi ya lugha 50 pamoja na nakala zaidi ya milioni 20 zilizochapishwa