-
Hakuna somo lenye umuhimu zaidi ya kuwa ndani ya mapenzi makamilifu ya Mungu. Kitu kimoja ambacho kitawatofautisha wahudumu wa injili ni uwezo wao wa kusikia sauti ya Mungu kwa usahihi. Ni jinsi gani ilivyo muhimu kufuata Roho Mtakatifu katika mapenzi makamilifu ya Mungu. Pale unapokuwa ndani ya mapenzi makamilifu ya Mungu, utastawi na kufikia yote unayotamani kwa ajili ya Mungu. Kazi hii bora ya Dag Heward- Mills itakuwa na mguso mkubwa sana katika maisha yako na huduma yako. -
Ingawa ni hitajiko la Mungu la kimsingi kwa viongozi, wachache sana wameandika kuhusu suala hili. Katika kitabu hiki, Dag Heward-Mills anaainisha misingi muhimu sana na kusudi la kuongeza uthabiti wa makanisa. Maudhui ya kitabu hiki ni husiani na ya vitendo mno jinsi kwamba yamekuwa zana zisizotupika kwa viongozi wengi wa kanisa. -
Ni nini jukumu kuu la mchungaji? Je, ni kufanya mazishi na kusimamia harusi? Kamwe sio! Haya ni majukumu ya mtumishi lakini sio majukumu kuu. Ikiwa utumishi wako umezorota hadi majukumu yako kuu ni kuendesha harusi na kuzika watu, basi unafaa kusoma Biblia yako tena! Jukumu kuu la mtumishi ni kutimiza Utume Mkuu. -
Dag Heward-Mills ni mwandishi wa vitabu vingi, ikiwemo kitabu kinachouzwa sana "Uaminifu na Ukosefu wa Uaminifu". Yeye ni mwanzilishi wa dhehebu lenye makanisa zaidi ya elfu moja linaloitwa "The Lighthouse Chapel International". (Kanisa la Kimataifa la Lighthouse). Dag Heward-Mills, mwinjilisti wa kimataifa huhudumu katika Mkutano wa Injili wa Kimataifa na Yesu Mponyaji na mikutano duniani kote. kwa taarifa zaidi, tembelea www.daghewardmills.org. -
Kwa kweli Mungu amewaita watu wengi. Maisha yetu duniani ni fursa ya kumtumikia, na Mungu anaangalia vitu unavyofanya kwa ajili ya Ufalme wake. Kitabu hiki kinachagamsha usomaji. Ukihifadhi akilini mawazo ya ukweli yaliyoandikwa na mwandishi, utapokea hekima kutumia fursa ya maisha yako kwa njia sahihi. -
Dag Heward-Mills ni mwandishi wa vitabu vingi, ikiwemo kitabu kinachouzwa sana "Uaminifu na Ukosefu wa Uaminifu". Yeye ni mwanzilishi wa dhehebu lenye makanisa zaidi ya elfu moja linaloitwa "The Lighthouse Chapel International". (Kanisa la Kimataifa la Lighthouse). Dag Heward-Mills, mwinjilisti wa kimataifa huhudumu katika Mkutano wa Injili wa Kimataifa na Yesu Mponyaji na mikutano duniani kote. kwa taarifa zaidi, tembelea www.daghewardmills.org. -
Heshima ni jambo muhimu ambalo kila mtu anahitaji kujua. Kuheshimu ni amri ya kibiblia. Heshima ni muhimu sana katika uhusiano wako na Mungu. Heshima ni muhimu sana katika uhusiano wako na nabii wako, mchungaji wako, mume wako na watu wengine wenye mamlaka. Usipompa heshima anayestahiki heshima, kamwe hutakuwa na uhusiano sahihi na watu fulani. -
Yesu Kristo ndiye Nabii mkuu zaidi aliyepata kuishi! Alitabiri kwamba maumivu na makwazo yatakuja kwa kila mmoja. Maumivu na makwazo yamesababisha uharibifu mkubwa sana katika kanisa. Ni ombi langu kwamba kwa maneno haya machache utaokolewa kutoka kwa uovu na laana inayokuja kwa njia ya kwazo. Tena, zaidi ya hayo, mwanangu, uwe na maonyo: kutunga vitabu vingi hakuna mwisho; na kusoma sana ni uchovu wa mwili! -
Uasi si kosa tu - ni kosa kubwa machoni pa Mungu! Uasi ni roho inayokaidi mamlaka na kwenda kinyume na utaratibu uliowekwa na Mungu. Ni mzizi wa machafuko na unaweza kukuongoza kwenye kiza kinene cha maisha na huduma, ikiwa utairuhusu katika maisha yako! Kumbuka, uasi ulikuwa dhambi ya kwanza kuwahi kuandikwa katika Biblia! Uasi ulimchukua malaika wa nuru na kumbadilisha kuwa shetani. Hiyo ndiyo nguvu ya uasi! Ni hatari, ni yenye hila na itakuharibu ikiwa utairuhusu kuota mizizi ndani yako. Katika kitabu hiki, utagundua jinsi ya kutambua aina mbili za uasi zilizofichika na zilizo wazi ambazo zinaweza kuingilia maisha yako au huduma yako. Usichukulie kijuu juu! Viondoe miongoni mwenu!