Uasi si kosa tu – ni kosa kubwa machoni pa Mungu! Uasi ni roho inayokaidi mamlaka na kwenda kinyume na utaratibu uliowekwa na Mungu. Ni mzizi wa machafuko na unaweza kukuongoza kwenye kiza kinene cha maisha na huduma, ikiwa utairuhusu katika maisha yako!
Kumbuka, uasi ulikuwa dhambi ya kwanza kuwahi kuandikwa katika Biblia! Uasi ulimchukua malaika wa nuru na kumbadilisha kuwa shetani. Hiyo ndiyo nguvu ya uasi! Ni hatari, ni yenye hila na itakuharibu ikiwa utairuhusu kuota mizizi ndani yako.
Katika kitabu hiki, utagundua jinsi ya kutambua aina mbili za uasi zilizofichika na zilizo wazi ambazo zinaweza kuingilia maisha yako au huduma yako. Usichukulie kijuu juu! Viondoe miongoni mwenu!

Reviews
There are no reviews yet.