-
"Biblia inazungumzia aina nyingi za damu: damu ya mbuzi, damu ya kondoo, damu ya njiwa! Biblia pia inasema wazi wazi kwamba pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo la dhambi. Je, aina yoyote ya damu miongoni mwa damu hizi inaweza kuondoa dhambi zetu? Jibu ni 'Hasha!" "Sasa nini kinaweza kuosha dhambi zetu?" Hakuna kingine isipokuwa damu ya Yesu! Damu ya Yesu pekee ndiyo yenye nguvu za kuosha dhambi zetu na kuleta wokovu. Katika kitabu hiki muhimu sana, utagundua ukweli mwingi mtakatifu kuhusu damu ya Yesu Kristo. Utaona jinsi damu ya Yesu inavyotoa uzima na jinsi damu ya Yesu ilivyopata umuhimu wake. Utaelewa kuchangamana kwa Roho Mtakatifu na damu ya Yesu. Kwa kweli, kuna nguvu katika damu ya Yesu."
-
Dag Heward-Mills ni mwandishi wa vitabu vingi, ikiwemo kitabu kinachouzwa sana "Uaminifu na Ukosefu wa Uaminifu". Yeye ni mwanzilishi wa dhehebu lenye makanisa zaidi ya elfu moja linaloitwa "The Lighthouse Chapel International". (Kanisa la Kimataifa la Lighthouse). Dag Heward-Mills, mwinjilisti wa kimataifa huhudumu katika Mkutano wa Injili wa Kimataifa na Yesu Mponyaji na mikutano duniani kote. kwa taarifa zaidi, tembelea www.daghewardmills.org.
-
Usiku mmoja, wakati akiwa ni mwanafunzi wa utabibu katika mji mmoja huko Ghana, katika hali ya mwujiza Mungu alimpaka mafuta Dag Heward-Mills wakati alipokuwa akimsubiri Bwana. Alipakwa mafuta kwa namna isiyo ya kawaida na kusikia maneno, “Tangu sasa na kuendelea unaweza kufundisha…” Wito huu usio wa kawaida ndio uliomwongoza kwenye huduma iliyosambaa duniani kote.
-
"Kumfuata Mungu ni safari ya kusisimua ya ugunduzi. Kufuata na kuiga watu wengine ni sanaa za toka jadi za kujifunza ambazo Yesu Kristo alichagua kama kanuni yake kuu ya kufundisha watu. Badala ya kujitenga na mbinu hii ya kujifundisha ambayo imetumiwa kwa muda mrefu, ni wakati wa kuelewa uzuri na unyenyekevu uliyo katika sanaa ya kufuata. Katika kitabu hiki utagundua ni nani, ni nini na jinsi unavyopaswa kufuata kwa njia inayostahili. Kitabu hiki kipya na kizuri mno kilichoandikwa na Dag Heward-Mills kinaipatia sanaa ya kufuata nafasi yake inayofaa katika maisha yetu ya Kikristo."
-
Dag Heward-Mills ni mwandishi wa vitabu vingi, ikiwemo kitabu kinachouzwa sana "Uaminifu na Ukosefu wa Uaminifu". Yeye ni mwanzilishi wa dhehebu lenye makanisa zaidi ya elfu moja linaloitwa "The Lighthouse Chapel International". (Kanisa la Kimataifa la Lighthouse). Dag Heward-Mills, mwinjilisti wa kimataifa huhudumu katika Mkutano wa Injili wa Kimataifa na Yesu Mponyaji na mikutano duniani kote. kwa taarifa zaidi, tembelea www.daghewardmills.org.
-
Dag Heward-Mills ni mwandishi wa vitabu vingi, ikiwemo kitabu kinachouzwa sana "Uaminifu na Ukosefu wa Uaminifu". Yeye ni mwanzilishi wa dhehebu lenye makanisa zaidi ya elfu moja linaloitwa "The Lighthouse Chapel International". (Kanisa la Kimataifa la Lighthouse). Dag Heward-Mills, mwinjilisti wa kimataifa huhudumu katika Mkutano wa Injili wa Kimataifa na Yesu Mponyaji na mikutano duniani kote. kwa taarifa zaidi, tembelea www.daghewardmills.org.
-
Kujenga ustadi ni kujenga uwezo au ujuzi. Biblia inasema kwamba kibali huja kwa watu wenye ujuzi. Kazi ya huduma huhitaji uwezo mkubwa. Kitabu hiki kipya, "Stadi ya Huduma" ni rasiliamali inayohitajika sana kwa wale wote wanaotamani kufanya kazi ya huduma. Inawasilisha vizuri mawazo yapi ni sahihi na yapi ni mabaya kuhusu huduma, nini kazi ya huduma, ni kipi kinachotakiwa kwako kama mfanyakazi katika huduma na jinsi gani ya kufanya majukumu ya mtumishi. Je umewahi kuwaza jinsi ya kufanya kazi yako katika huduma? Kitabu hiki cha kipekee cha Dag Heward- Mills kitakupa changamoto kutembea kwa kulingana na wito wa Mungu na kukuongoza katika kujitoa kikamilifu katika kazi ya huduma.
-
Ikiwa wewe ni mchungaji wa kondoo za Mungu, utasaidiwa pakubwa na kazi hii iliyozingatiwa vyema. Kurasa hizi zina maelekezo ya kina na iliyochaguliwa kwa makini, muhimu kwa kufaulu. Kurasa hizi zina maelekezo ya kina na iliyochaguliwa kwa makini, muhimu kwa kufaulu. Dag Heward-Mills anatoa kutoka kwa tajriba yako ya uchungaji ya miaka thelathini, kugawa ufahamu kwa vitendo katika kazi ya utumishi.
-
Hakuna somo lenye umuhimu zaidi ya kuwa ndani ya mapenzi makamilifu ya Mungu. Kitu kimoja ambacho kitawatofautisha wahudumu wa injili ni uwezo wao wa kusikia sauti ya Mungu kwa usahihi. Ni jinsi gani ilivyo muhimu kufuata Roho Mtakatifu katika mapenzi makamilifu ya Mungu. Pale unapokuwa ndani ya mapenzi makamilifu ya Mungu, utastawi na kufikia yote unayotamani kwa ajili ya Mungu. Kazi hii bora ya Dag Heward- Mills itakuwa na mguso mkubwa sana katika maisha yako na huduma yako.
-
Ingawa ni hitajiko la Mungu la kimsingi kwa viongozi, wachache sana wameandika kuhusu suala hili. Katika kitabu hiki, Dag Heward-Mills anaainisha misingi muhimu sana na kusudi la kuongeza uthabiti wa makanisa. Maudhui ya kitabu hiki ni husiani na ya vitendo mno jinsi kwamba yamekuwa zana zisizotupika kwa viongozi wengi wa kanisa.
-
Ni nini jukumu kuu la mchungaji? Je, ni kufanya mazishi na kusimamia harusi? Kamwe sio! Haya ni majukumu ya mtumishi lakini sio majukumu kuu. Ikiwa utumishi wako umezorota hadi majukumu yako kuu ni kuendesha harusi na kuzika watu, basi unafaa kusoma Biblia yako tena! Jukumu kuu la mtumishi ni kutimiza Utume Mkuu.